"GB 1 unapewa MB 800" Spika amcharukia Waziri; Vifurushi vya bando vyazua kizaa zaa Bungeni
Mbunge wa jimbo la Nkalama (CCM) Francis Ntenga amelalamikia suala la muda wa vifurushi vya Simu (Bando) kuisha wakati mtumniaji hajamaliza kifurushi chake na kutaka sheria inayoruhusu jambo hilo ibadilishwe. "Simu ni ya kwangu na nanunua bando kwa fedha yangu halafu unanilazimisha nitumie kwa muda unaotaka wewe, kama ni sheria iletwe hapa tuibadilishe kwasababu tunawaibia wananchi" Aliongeza Ntenga Akitoa taarifa kuhusu jambo hilo Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye amesema kuwa huo ni utaratibu wa kawaida wa biashara. Aidha Spika wa Bunge Dk Tulia Ackson amemtaka Waziri Nape wakati wa kuhitimisha hoja atakapopata muda wa kuchangia atoe kauli juu ya wale ambao wamekuwa wakitengeneza mazingira ambayo wananchi wamekuwa wakihisi kuwa wanaibiwa.